Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), kimeendelea kutoa elimu kwa jamii ili kusaidia kuleta mageuzi chanya ya kiuchumi. Elimu imetolewa kupitia semina ilifanyika tarehe 03 Novemba 2023, Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Dkt. Lohoya Chamwali (aliyezungumza kwa niaba ya Kaimu Mratibu wa Mradi wa HEET Chuo Kikuu Mzumbe) ameeleza lengo la semina hiyo ni kuisaidia jamii kupunguza umasikini kwa uchaguzi wa nishati sahihi za kupikia.

Semina hii ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Watafiti kutoka Kitivo cha Sayansi ya Jamii chini ya uratibu wa HEET upande wa kukuza uwezo wa utafiti na ubunifu tumishi unaoratibiwa na Dkt. Christina Shitima, na usaidizi wa Kurugenzi ya Huduma za Umma.

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka idara ya Uchumi, Kitivo cha Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu Mzumbe na Mwezeshaji wa Semina hiyo, Dkt. Felister Y. Tibamanya, wakati wa uwasilishaji wa mada yake, aliwasilisha alibainisha aina za nishati na athari zake ili kujenga uelewa kwa wanasemina.

Aidha, Mhadhiri Msaidizi kutoka idara ya Mazingira na Maendeleo Endelevu katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo (IDS) Chuo Kikuu Mzumbe na Mwezeshaji mwingine wa Semina hiyo, Bi. Elihaika K. Joseph alieleza namna nishati isiyofaa inaweza kusababisha umasikini.

Katika wasilisho lingine, Mkufunzi Msaidizi kutoka idara ya Uchumi, Kitivo cha Sayansi za Jamii Chuo Kikuu Mzumbe na Mwezeshaji wa Semina, Bi. Nyamsabi Nyamwero, alifafanua nishati ambazo ni rafiki wa mazingira, zenye gharama nafuu na zisizo na madhara makubwa katika afya.

Katika kuhitimisha semina hiyo, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Changarawe, Bi. Teddy S. Eustach, kwa niaba ya viongozi hao, ametoa shukrani kwa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuona umuhimu wa kuandaa semina hiyo. Bi. Teddy ameomba semina za namna hiyo ziendelee ili kuwafikia wananchi ambao wataelimika na kuona umuhimu wa matumizi ya nishati sahihi na itakayosaidia kupunguza umasikini kwa jamii.

Karibu Chuo Kikuu Mzumb, “Tujifunze Kwa Maendeleo ya Watu”

*****************************

Kwa picha zaidi za semina hii,Tembelea ukurasa wetu wa Facebook,Bofya hapa

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top