Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha leo tarehe 10 Februari 2024 ameongoza jumuiya wa wanamzumbe katika zoezi la upandaji miti katika eneo la Maekani.
Akizungumza kabla ya zoezi hilo Prof. Mwegoha amesema Chuo Kikuu Mzumbe kinaunga mkono maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha zoezi la upandaji miti linakuwa endelevu.
"Hili ni zoezi endelevu, tunaunga mkono maelekezo ya Mhe. Rais na leo hii tunapanda miti 3000 katika eneo hili.k Tunaendelea kutunza mazingira, sisi kazi yetu kuhakiksha tunalinda bioanuai" amesisitiza Prof. Mwegoha.
 
Katika kuhakikisha miti iliyopandwa inakuwa na kustawi, Prof. Mwegoha amesema kupitia Kamati ya Mazingira wamejipanga kuwa na usimamizi endelevu na kuhakikisha miti inakuwa.
Awali, Prof. Allen Mushi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala ametoa rai kwa jamii kuhakikisha wanapanda miti na kuitunza na kuepuka uchomaji holela wa misitu.
"Kupanda miti ni kuhimu sana, Tupande miti na kuitunza, tusichome moto ovyo" amesisitiza Prof. Mushi.
 
Akitoa shukrani kwa niaba ya wadau walioshiriki katika zoezi hilo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Utafiti na Ushauri Prof. Eliza Mwakasangula amesema azma ya Chuo Kikuu Mzumbe ni kupanda miti takribani elfu ishirini ambayo itapandwa kwa awamu katika eneo la Maekani.
Zoezi la upandaji miti lilitanguliwa na mazoezi ya viungo yaliyoshirikisha klabu za mazoezi, wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Wanafunzi wa Shule za Sekondari, Benki ya CRDB, NMB na watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe na jamii ya Kijiji cha Changarawe.
 
********************************
 
 
Kwa Picha zaidi za tukio hili,tembelea kurasa zetu za mitandao ya Kijamii.
 
 
 
Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top